Wakimbizi wa Kisomali wanaoingia Kenya waanza kupungua lakini adha bado zipo

20 Aprili 2012

Machafuko ambayo yamelikumba taifa la Somalia kwa zaidi ya miongo miwili sasa na yamesababisha kuhama kwa wananchi wengi wa taifa hilo la pemba ya Afrika na kuwa wakimbizi kwenye mataifa jirani huku wengine wakihamia mataifa ya mbali hasa barani Ulaya na Marekani.

Hata hivyo taifa jirani la Kenya limeshuhudia idadi kubwa zaidi ya wakimbizi kutoka Somalia ambao wengi wao wanaishi kwenye kambi za Daadab na Kakuma huku kambi ya Dadaab ikitajwa kuwapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 400,000 ambao ni wengi zaidi kuliko kambi yoyote ile duniani.

Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi ameandaa makala kuhusu hali ya sasa ya wakimbizi kwenye kambi za Dadab na Kakuma na pia athari za wakimbizi kutoka Somalia waliohamia miji ya Kenya hasa mji mkuu Nairobi. Ungana naye.

(PKG BY JASON NYAKUNDI)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud