Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yakaribisha muongozo mpya unaotoa msaada zaidi kwa wanandoa wenye HIV waliofarakana

UNAIDS yakaribisha muongozo mpya unaotoa msaada zaidi kwa wanandoa wenye HIV waliofarakana

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi UNAIDS limekaribisha muongozo mpya kwa wanandoa kuhusu upimaji wa virusi vya HIV, ushauri nasaha na upewaji wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi kwa wanandoa wanaoishi na virusi vya HIV ili kupunguza hatari ya kuwaambukiza virusi wenzi wao.

Muongozo huo mpya umetolewa ili kuwatia moyo wanandoa kwenda pamoja kupima virusi ili kujua hali zao za HIV. Muongozo huo uliotolewa na shirika la afya duniani WHO pia umependekeza kwamba wanadoa walio katika mfarakano na ambapo mmoja wao anaishi na virusi vya HIV na mwingine hana , dawa za kupunguza makali ya ukimwi apewe anayeishi na virusi ili kuzuia mwenzi wake kuambukizwa.

UNAIDS imetoa wito kwa nchi zote kutekeleza muongozo huo ili kufikia malengo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2011 ambayo ni azimio la kisiasa kuhusu vita dhidi ya ukimwi. Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe amesema muongozo huo unatoa fursa kwa wanandoa kufaidia na ARV’s , kuimarisha afya zao na kuwalinda wenzi wao.