Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka mataifa kupunguza matumizi kwenye maeneo ya kijeshi na kusaidia shughuli za maendeleo

UM wataka mataifa kupunguza matumizi kwenye maeneo ya kijeshi na kusaidia shughuli za maendeleo

Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na usalimishaji wa silaha amewapa shime viongozi wa dunia kutupia macho mienendo yao ya ufadhili kwenye maeneo ya ulinzi wa kijeshi na kisha kuanza kufiria kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba vipaumbele zaidi vinawekwa kwenye maeneo ya maendeleo kwa mustakabala mwema wa dunia.

Afisa huyo Angela Kane amesema viongozi wa dunia wanaweza sasa kuchukua mkondo mpya vya kuhamisha vipaumbele vya kufadhilia shughuli za kijeshi na badala yake mafungu ya fedha zaidi yakaelekezwa kwenye maeneo ya ujenzi wa mifumo ya kijamii na kusuma mbele maendeleo kwa ujumla.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa juu ya matumizi kwenye maeneo ya kijeshi, Kane amesema kuwa dunia imetupia macho zaidi kwa kudisha matumizi kwenye maeneo ya jeshi huku ikipuzilia maeneo mengine ambayo amesema kuwa yakifadhiliwa vyema yanaweza kutoa mchango mkubwa kwa usalama wa dunia.

 Nchi nyingi zilizoendelea zinatajwa kutenga mafungu makubwa ya bajeti kwenye maeneo ya kijeshi jambo ambalo wakosoaji wa mambo wanasema kuwa kiasi hicho cha fedha kingeweza kutumika kukabiliana na tatizo la umaskini linalokabili mataifa mengi duniani.