Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kudhibiti maambukizi ya HIV Afrika ni muhimu katika kukabiliana na athari za muda mrefu:Benki ya dunia

Kudhibiti maambukizi ya HIV Afrika ni muhimu katika kukabiliana na athari za muda mrefu:Benki ya dunia

Bila kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya HIV Afrika mipango iliyopo ya kitaifa ya kupambana na ukimwi haitoweza kuendelea kwa siku za usoni imeonya ripoti mpya ya Bank ya dunia. Ripoti imezitaka serikali za Afrika, washirika wa maendeleo na wahisani kuongeza juhudi zao za kuzuia maambukizi ya HIV ili kuzuia tatizo hilo la kutohimili mipango kutokea.

Vita dhidi ya HIV na ukimwi nchini Botswana, Afrika ya Kusini, Swaziland na Uganda vimepiga hatua huku watu takribani milioni 6 hivi sasa wanapata dawa za kupunguza makali ya ukimwi na matumizi ya ukimwi yameongezeka duniani kutoka dola milioni 300 mwaka 1996 na kufikia karibu dola bilioni 16 mwaka 2009.

Hata hivyo ripoti inaelezea ongezeko la haraka la gharama za matibabu ya ukimwi na athari zake kwa masuala ya fedha kwa umma ambao tayari una mzigo mkubwa.

Kwa mujibu wa Elizabeth Lule mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo mikakati imara ya uwekezaji katika kuzuia maambukizi ya HIV wakati pia wakitimiza mahitaji ya sasa ya tiba, msaada na huduma kunaweza kuzisaidia nchi kupanga mipango ya kuepuka mzigo ambao unaweza kuwa vigumu kuubeba.