UNESCO yataka urithi wa nyaraka za Timbuktu ulindwe

16 Aprili 2012

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova Jumatatu amezungumzia kuhusu usalama wa kituo cha urithi wa kitamaduni cha Timbuktu nchini Mali, kufuatia ripoti kwamba waasi wamekivamia na kupora. Kituo hicho kinahifadhi maelfu ya vitabu vya kihistoria na nyaraka zinazoelezea historia ya mji huo.

Bi Bokova ameutaka uongozi wa Mali ikiwemo makundi ya waasi, serikali za jirani, Interpol, mashirika ya kitamaduni, masoko ya vitu vya kihistoria na wanaokusanya sanaa za kihistori kuwa makini dhidi ya jaribio lolote la kusafirisha kiharamu vitu vilivyoibiwa kutoka katika kituo cha Timbuktu. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter