Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yasema itaanza kuondoa vikosi katika maeneo ya raia

Syria yasema itaanza kuondoa vikosi katika maeneo ya raia

Serikali ya Syria imesema itaanza kuondoa vikosi vyake katika maeneo ya raia ili kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiaarabu Kofi Annan.

Taarifa za kuanza kuondoka kwa vikosi hivyo zimeripotiwa katika miji ya Daraa, Idlib na Zabadani.

Shughuli ya kuondoka kabisa kwa vikosi hivyo inatarajiwa kukamilika Aprili 10 na itafuatia na kipindi cha saa 48 za kusitisha kabisa ghasia na mapigano kwa wote, vikosi vya serikali na majeshi ya upinzani.

Mwakilishi maalumu amependekeza kupelekwa kwa mpango wa kuulinda amani ili kusimamia na kuangalia zoezi la usitishaji mapigano.

Ahmed Fawzi ni msemaji wa mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu nchini Syria.

(SAUTI YA AHMED FAWZI)

Bwana Annan leo pia atatoa taarifa kwenye baraza kuu la Umoja wa mataifa kuhusu hatua zilizopigwa na mpango wake wa kuleta amani nchini Syria.