Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria inahitaji kupewa 'kidogo kidogo' amesema Annan

Syria inahitaji kupewa 'kidogo kidogo' amesema Annan

Ghasia zilizoko Syria haziwezi kutatuliwa kupitia njia ya kitamaduni ya kutuma ujumbe kati ya majeshi mawili hii ni kwa mujibu wa tume maalamu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi za kiarabu.

Kofi Annan ameliambia Baraza Kuu kwamba timu ya Umoja wa Mataifa ili wasili nchini Syria Alhamisi kuanza maandalizi ya uwezekano wa kupelekwa kwa wasimamizi kusimamia kusitishwa kwa ghasia na makundi yaliojihami na kutekeleza mpango ulio pendekezwa.

Bw. Annan aliyearifu UM kuhusu juhudi za kidiplomasia za kuhakikisha utekelezaji wa pointi 6 zitakazopelekea kutatua mzozo nchini alisema hali ilivyo nchini Syria inayoyoma na hakuna mwongozo imara na amani haitapatikana bila kuwepo kwa mchakato wa kwaminika wa kisiasa.

(SAUTI YA ANNAN)

Kile tunahitaji mashinani ni uwepo wa UM kwa kiasi tu. Itahitajika kupeleka ujumbe kwa haraka kwa mamlaka pana na rahisi. Uhuru wake wa kutembea kote nchini unapaswa kuhakikishwa. Inapaswa kuhusisha vikundi vyote, Inapaswa kuangalia mara kwa mara na kuweka ma kuchunguza ukweli na hali ilivyo mashinani bila mapendeleo.