Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kuondolewa kwa mabomu ya ardhini

Ban ataka kuondolewa kwa mabomu ya ardhini

Serikali kote duniani zimetakiwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kuondoa mabomu ya ardhini yaliyoachwa wakati wa vita  kwa lengo la kuufanya ulimwengu kuwa salama.

Haya yamesemwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na katika ukusanyaji wa mabomu hayo.

Ban amesema kuwa kwenye siku hii wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa wanashiriki kwenye kampeni ya kuonyesha uzalendo kwa wahanga wa ajali za  mabomu ya ardhini.