Raia wa Chad waliorejea nyumbani wanahitaji msaada:IOM

30 Machi 2012

Uchunguzi wa IOM kwa wahamiaji kutoka Chad waliorejea kutoka Libya inasema kwamba wengine wanahitaji msaada wa dharura kuunganishwa na jamii zao.

Uchunguzi huo pia uligundua kuwa waliorejea nyumbani wamekumbana na changamoto zikiwemo za  kifedha za kujitafutia  na kwa familia zao.

Uchunguzi huo uliendeshwa kati ya Januari na Machi mwaka huu kwenye maeneo 14 nchini Chad yaliyo na idadi kubwa ya watu waliorejea nyumbani na uliwahoji watu 1000 waliorejea nyumbani.

Wengi wanasema wanapata changamoto za kuishi na familia zinazowapa makao kutokana na tofauti ya lugha, ukosefu wa kazi na huduma zingine.

Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Karibu raia 90,000 waliorejea nyumbani wameishi nchini Libya kwa miaka mingi na hawana uhusiano wa karibu  na maeneo walikotoka.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter