Skip to main content

UNHCR yakaribisha hatua ya Umoja wa Ulaya kuridhia mpango wa makazi

UNHCR yakaribisha hatua ya Umoja wa Ulaya kuridhia mpango wa makazi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuridhia mpango maalumu wa uwekaji makazi

Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kuwa hatua hiyo inatoa matumaini na ishara njema kwa jinsi ambavyo Umoja huo na wanachama wake walivyotayari kusaidia mkwamo wa makazi unaoikabili dunia kwa sasa.

Nchi 12 wanachama wa Umoja huo kwa hivi sasa zinaendesha mpango wa utoaji makazi na hivyo kuchangia kwa asilimia 8 kila mwaka katika juhudi za dunia kwa ujumla kuhusiana na utoaji makazi.

Kupitia mpango raia kutokana nchi kadhaa ulimwenguni hasa lakini kutoka Afghanistan, Jamhuri ya watu wa Congo DRC, Eritrea, Iraq, Myanmar na Somalia wanapewa vipaumbele vya pekee kuingia katika nchi za Ulaya zilizoridhia kwa hiari mpango huo.