Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uwezekano mdogo wa kuendelea na mpango wa amani mashariki ya kati:Serry

Kuna uwezekano mdogo wa kuendelea na mpango wa amani mashariki ya kati:Serry

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Mashariki ya kati Robert Serry amesema kuwa hali kati ya Wapalestina na Waisrael inasalia kuwa isiyotabirika na ngumu.

Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Serry amesema kuwa kilichoko ni kwamba pande zote mbili hazijapa makubaliano ya kurejea kwenye mazungumzo na uwezekano huo unasalia kuwa mdogo.

Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Isreal na Wapalestina yalikwama mwaka 2010 baada ya ya Israel kukataa kuongeza muda wa usitishaji wa ujenzi wa  makao ya walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya Wapelstina iliyonyakuliwa.