Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walinda amani wana wajibu wa kuhakikisha amani inaendelea hata wakiondoka:Ladsous

Walinda amani wana wajibu wa kuhakikisha amani inaendelea hata wakiondoka:Ladsous

Walinda amani wana wajibu wa kuhakikisha amani inaendelea kwa muda mrefu hata baada ya kuondoka eneo lenye vita amesema afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa.

Akitoa taarifa kwenye baraza la usalama Jumatatu Herve Ladsous ambaye ni mkuu wa idara ya operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa amesema kuondoka kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa sio suala la kupunguza idadi ni majukumu makubwa zaidi ya hapo.

 (SAUTI YA HERVE LADSOUS)

Ladsous amesema kuondoka kwa walinda amani lazima kuwe kwa hatua baada ya kufanyika kwa tathimini ya kina, majadiliano na wadau wa kitaifa na kimataifa na kuhakikisha uwezo wa nchi kubeba jukumu la kudumisha amani.