Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia itizame upya agenda zake za kimaendeleo

Dunia itizame upya agenda zake za kimaendeleo

Jumuiya ya kimataifa imeshawishiwa kuweka upenyo wa pamoja ili kushagihisha agenda za maendeleo ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endeleo.

Wakishiriki kwenye mkutano wa kimataifa unaoratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa ushirikiano na Uturuki, wajumbe kwenye mkutano huo wametoa wito kwa jumuiya kimataifa kuzitizama upya agenda zinazogusia maendeleo kwa kiu moja ya kuwa na maendeleo endelevu.

 Mkutano huo unawajumuisha jumla ya wajumbe 200 kutoka kona mbalimbali duniani ikiwemo vyama vya kiraia, wataalamu wa masuala ya maendeleo, wawakilishi wa mashirika binafsi na maafisa wa Umoja wa Mataifa.

Katika risala yake kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa  suala la maendeleo endelevu haliwezi kufikiwa kwa kuwa na sera zinazopishana kwenye maeneo ya uchumi, jamii na mazingira.

Ametaka kuwepo uwiano wa mambo ili hatimaye lengo hilo linafikiwa.