Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na viongozi wa Australia na Gabon kwenye mkutano wa nyuklia

Ban azungumza na viongozi wa Australia na Gabon kwenye mkutano wa nyuklia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko Seoul Korea kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia amefanya mazungumzo kando na mkutano na baadhi ya viongozi wa dunia.

Ban alipozungumza na waziri mkuu wa Australia Julia Gillard ameishukuru nchi hiyo kwa mchango wake mkubwa kwa kazi za Umoja wa mataifa na hasa katika masuala ya kibinadamu, maendeleo, mipango ya kulinda amani na masuala ya kisiasa.

Wamejadili pia usalama wa nyuklia na maandalizi ya mkutano wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa Rio+20.

Jumapili jioni Ban amefanya mazungumzo na Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon ambapo wamejadili hali ya Gabon na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Viongozi hao wawili wameahidi kuimarisha ushirikiano kati yao hasa kwa kuzingatia kwamba Gabon ndiko kuliko na ofisi mpya ya mpango wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika ya Kati UNOCA.

Jambo lingine walilotilia manaani ni kuitisha mkutano wa pamoja utakaoshirikisha ECCAS, ECOWAS na tume ya ghuba ya Guinea ili kuanzisha mkakati wa pamoja wa ulinzi wa baharini.