Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mrembo wa ulimwengu 2011 kuelimisha kuhusu maeneo kame

Mrembo wa ulimwengu 2011 kuelimisha kuhusu maeneo kame

Mwanamke mrembo kabisa ulimwenguni atasaidia kuelimisha kuhusu kuporomoka kwa maeneo kame, tatizo ambalo linaathiri zaidi ya watu bilioni moja duniani.

Mrembo wa ulimwengu mwaka 2011 Leila Lopes ameteuliwa kuwa balozi mwema wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na hali ya jangwa (UNCCD).

Akizungumza mjini New York Jumatatu Bi Leila Lopes amesema maeneo makame sio ardhi ya kupoteza na yanaweza kuokolewa. Amesema endapo tatizo hilo likishughulikiwa basi tunaweza kukabiliana na umasikini katika njia muafaka kwa sababu kila dakika tunapoteza ekari 23 la ardhi kutokana na mmomonyoko.

Bi Lopez anataka kuwe na makubaliano ya malengo ambayo yatasaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo na kuokoa zaidi ardhi ambayo imeharibika na mmomonyoko.

Leila Lopes, ambaye anatoka nchini Angola, atashiriki pia katika shughuli mbalimbali za maandalizi ya kuelekea mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20 utakaofanyika Juni nchini Brazil .