Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na benki ya ADB kuzisaidia nchi zilizokumbwa na mapigano

UM na benki ya ADB kuzisaidia nchi zilizokumbwa na mapigano

Kamishna wa UM juu ya ujenzi wa amani kwa kushirikianan na benki ya maendeleo ya Afrika ADB zimeanza kutupia macho maeneo ambayo yalikumbwa na machafuko ya vita barani Afrika.

Balozi Eugène-Richard Gasana ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa bodi amesema kwamba pande zote mbili zinaimarisha mikakati ya namna ya kuzisaidia nchi zilizopitia katika mizozo.

Pande hizo zitafanya kazi kwa pamoja kusaka vitendo vya kazi na wakati huo kusaka njia ya majadiliano yatakayohusisha maeneo yaliyoathiriwa na machafuko.

Kamishna hiyo ya UM iliundwa mwaka 2005 kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika zilizopita katika machafuko ya vita.

Kwa hivi sasa kamishna hiyo inashughulikia nchi sita.

Nchi hizo ni pamoja na Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati Guinea, Guinea Bissau, Liberia, na Sierra Leoni.