Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yashangazwa na mashambulizi ya mabomu mjini Mogadishu

UNHCR yashangazwa na mashambulizi ya mabomu mjini Mogadishu

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasi wasi wake kutokana na mashambulizi ya mabomu ambayo yamewaua watu wanne siku za hivi majuzi mjini Mogadishi nchini Somalia.

Mabomu yalianguka eneo wanakopiga kambi wakimbizi wa ndani kwenye wilaya ya Wardhigley mapema hiyo jana.

Inaripotiwa kuwa hadi wakimbizi wanne wa ndani wakiwemo watoto waliuawa.

Inaaminika kuwa shambulizi hilo lilikuwa likilenga wanakoishi wanajeshi wa seriakali pamoja na ikulu ya rais.

Hata hivyo mabomu hayo hayakufika yalikolengwa na badala yake yalianguka mahali walipokuwa wakimbizi wa ndani.

Hili ndilo shambulizi la kwanza tangu Agosti mwaka uliopita tangu makundi yanayoipinga seikali kuondoka kwenye sehemu nyingi za mji wa Mogadishu.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)