Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulikuwa na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye uchaguzi mkuu nchini DRC:UM

Kulikuwa na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye uchaguzi mkuu nchini DRC:UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo imetolewa hii leo inaonyesha kuwa kumekuwa na ukiukaji wa haki za binadamu yakiwemo mauaji, kutoweka kwa watu na kufungwa vyote vilivyotekelezwa na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati wa kura za urais na ubunge mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inayotokana na uchunguzi uliofanywa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuuawa kwa watu 33 mjini Kinshasa na vikosi vya usalama kati ya tarehe 26 mwezi Novemba na tarehe 21 mwezi Disemba mwaka uliopita.

Pia ripoti hiyo inaeleza kuwa watu 83 walipata majereha kwa njia ya risasi huku 16 wakiwa hawajulikani waliko.

Pia watu 265 waliikamatwa na wengi kufungiwa kwenye vituo kadhaa mjini Kinshasa ambapo inaaminika kulifanyika mateso.

Scott Campbell ni mkuu wa ofisi ya haki za binadamu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

(SCOTT CAMPBELL)