Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya Bahrain vinatumia nguvu kupita kiasi:UM

Vikosi vya Bahrain vinatumia nguvu kupita kiasi:UM

 

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa imepokea ripoti za kutia wasi wasi zinazohusu matumizi ya nguvu kutoka kwa wanajeshi wa Bahrain hasa matumizi wa gesi ya kutoa machozi na risasi na mipira dhidi ya waandamanaji.

Ripoti zinasema kuwa matumizi ya gesi ya kutoa machozi kumesababisha vifo vya waandamanaji kadha na idadi hiyo imekuwa ikipanda miezi michache iliyopita.

Pia taarifa zinasema kuwa raia waliokufa walipata matatizo ya kupumua baada ya vikosi vya usalama kufyatua vitoa machozi kwenda kwa umati wa watu.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema kuwa watu 30 wameuawa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita.