Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la Syria limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya kimataifa:Ban

Suala la Syria limekuwa tatizo kubwa kwa jamii ya kimataifa:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa hali nchini Syria kwa sasa imekuwa ya kutatiza na ni suala ambalo linaloisumbua jamii ya kimataifa.

Ban aliyasema haya kwenye mkutano na waandishi wa habari alioufanya na rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono.

Ban amesema kuwa  hata kama watu wa Syria wamepitia magumu wamekuwa wakisema na kuitisha kwa ujasiri haki zao zikiwemo haki za kusema.

Ban anasema kuwa anaamini jamii ya kimataifa itaendelea kuongea kwa sauti moja hasa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.