Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awasilisha ripoti ya jopo la kuhusu udhabiti wa dunia

Ban awasilisha ripoti ya jopo la kuhusu udhabiti wa dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amewasilisha ripoti ya jopo lake kuhusu udhabiti wa dunia yenye kichwa “Watu Imara, Sayari Imara: Siku za baadaye zilizo zenye maana”.

Lengo la jopo hilo ni kuangamiza umaskini na kupunguza ukosefu wa usawa ili kuchangia kuongezeka kwa uzalishaji na matumzi na pia kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti hiyo inatoa mapendekezo 56 jinsi ya kutekelezwa kwa malengo hayo kupitia kuwawezesha watu kufanya maamuzi ya kudumu na kuboreka kwa uchumi.

Ripoti hiyo inasistiza kuwa kuna fursa nyingi kwa watu, serikali na kwa biashara zinazoweza kuchangia katika kuboresha maisha ya baadaye.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)