Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanawake kwenye masuala ya kisiasa bado ni ya chini

Idadi ya wanawake kwenye masuala ya kisiasa bado ni ya chini

Chama cha bunge IPU kinasema kuwa hata kama mwaka 2011 ulishuhudia mabadiliko makubwa ya kisiasa na mabadiliko ya kidemokrasia kwenye sehemu tofauti za dunia, mwaka huo hata hivyo ulishuhudia idadi ndogo ya wanawake walioshiriki kwenye siasa.

Nchi kama Nicaragua, Ushelisheli, Slovenia, Andora na Uganda zilipiga hatua kubwa katika uwakilishi wa wanawake kwenye masuala ya siasa.

IPU inasema kuwa idadi ya wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa hivi majuzi nchini Misri ilipungua kutoka aslimia 12.7 hadi chini ya asilimia 2 na ni wanawake 10 tu waliochaguliwa kama wabunge kwenye bunge la wabunge 508.