Mwaka 2011 ulikuwa changamoto kubwa kwa haki za binadamu:Pillay

2 Machi 2012

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa mwaka 2011 ulikuwa ni mwaka wa changamoto nyingi kwa upande wa haki za binadamu hasa kutokana na hali mbaya ya uchumi duniani, hali mbaya ya hewa na uhaba wa chakula , njaa kwenye pembe ya Afrika, mizozo, ukabila na umaskini.

Amesema pia kuwa huu ni mwaka ambao ulishuhudia kuibuka kwa makundi yaliyopinga tawala dhalimu hasa kwenye eneo la mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika akiongeza kuwa nchi zilipigania usawa na uhuru kupitia ghasia na dhuluma. Huku ghasia hizo zikiendelea nchini Syria Pillay ameongeza kuwa jamii ya kiamataifa inastahili kuchukua hatua za dharura ili kuzua umwagikaji wa damu nchini himo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter