Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuongeza shinikizo kukomesha mila ya Ukeketaji

UM kuongeza shinikizo kukomesha mila ya Ukeketaji

 

Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa Angelique Kidjo anatazamiwa kutumbuiza kwenye tamasha maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kutokomeza vitendo vya ukeketaji.

Mwanamuziki huyo atapanda jukwaani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kutoa ujumbe unaohamasisha kukomeshwa kwa vitendo hivyo.

 Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya wasichana na wanawake milioni 140 wamekeketwa na kuna wasiwasi pia wasichana wengine kiasi cha milioni 3 wako hatarini ya kufanyiwa vitendo hivyo kila mwaka.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa vitendo vya ukeketaji vimebeba madhara yote, yale ya muda mfupi na muda mrefu pia. Akielezea tamasha hilo, Kidjo amesema kuwa ujumbe mkubwa utaotumwa kwa mataifa ya Afrika na maeneo mengine ambayo bado yanakumbatia desturi hiyo ni kuwataka waache kufanya hivyo.

(SAUTI YA ANGELIQUE KIDJO)