Ukaliwaji na watu wa nje hauendani na demokrasia: Nassir

27 Februari 2012

Ukaliwaji na watu wa nje unakwenda kinyume na demokrasia na haki za binadamu hususani haki ya kujitawala amesema Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser alipokuwa akilihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Jumatatu.

Amesema hali inayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu isisababishe kupuzwa kwa masuala ya amani na utlivu.

Ametaka juhudi zifanyike kuhakikisha Wapalestina wanakuwa huru na taifa lao na uhuru unapatikana kwa Wasyria waishio katika eneo linalokaliwa na milima ya Golan.

(SAUTI YA NASSIR AL-NASSER)

Ameongeza kuwa kuna mshikamano na muafaka wa kimataifa kuhusu haja ya haraka kuhakikisha ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi unasita.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter