Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Senegal yasubiri matokeo ya awali ya uchaguzi

Senegal yasubiri matokeo ya awali ya uchaguzi

Hali ya wasiwasi bado imetanda kufuatia Senegal kufanya uchaguzi wa Rais wa duru ya kwanza mwishoni mwa juma. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani barani Afrika amesema ana matumaini kwamba uchaguzi huo utakuwa ni huru, wa wazi, wa amani na unaoheshimu matakwa ya watu wa taifa hilo.

Kampeni za uchaguzi huo zilighubikwa na ghasia na maandamano katika mji mkuu Dakar na miji mingine. Waandamanaji wamearifiwa kukasirishwa na kitendo cha Rais aliyeko madarakani Abdoulaye Wade kutaka kuchaguliwa tena katika muhula wa tatu.

Duru za habari zinasema kwamba matokeo ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi huo wa Rais yanatarajiwa kutolewa karibuni na tume ya taifa ya uchaguzi.