Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA ina miradi ya kusaidia watu kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati

OCHA ina miradi ya kusaidia watu kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limesema kuwa suala la kibinadamu lizalosababishwa na mzozo kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati ndilo lililosahaulika zaidi barani Afrika linalopokea chini ya asilimia 50 ya ufadhili.

IOM kwa ushirikiano na serikali na washirika wengine wa kibinadamu wametoa ombi la kufadhili miradi 105 itakayochukua muda wa miezi 12. Hatua hii inalenga kuokoa maisha ya watu wanaokabiliwa na mizozo huku miradi hiyo ikiwa nalengo la kusaidia watu 1.9 . Hadi sasa Jamhuri ya Afrika ya Kati imepokea asilimia nne tu ya fedha ilizoomba.