Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jinsi suluhu ya mgogoro wa Syria inavyochelewa, maisha ya watu yanazidi kupotea:Ban

Jinsi suluhu ya mgogoro wa Syria inavyochelewa, maisha ya watu yanazidi kupotea:Ban

Mgogoro unaokumba nchi ya Syria Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anaendelea kutoa hofu na kiwango cha ghasia na ongezeko la kupotea kwa maisha ya watu nchini Syria.

Kwa mara nyingine Ban ameitolea wito serikali ya Syria kutekeleza sheria za kimataifa mara moja na kukomesha mashambulizi na matumizi ya nguvu dhidi ya raia. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Vienna Ban amesema jinsi suluhu ya machafuko ya Syria inavyozidi kuchelewa ndivyo maisha zaidi ya watu yanavyoendelea kupotea.

Amesema dunia inashuhudia ukiukaji mkubwa wa haki ukifanyika Syria, mashambulizi yanayolenga makundi ya watu kadhaa, hospitali zikitumika kama vituo vya utesaji, watoto wakifungwa na ukatili mwingine unaokwenda kinyume na haki za binadamu.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)