Mihadarati ni tishio kwa maendeleo ya Afghanistan na jirani zake:Ban

16 Februari 2012
Ban Ki-moonAfghanistan inakabiliwa na moja ya matatizo makubwa ya matumizi ya kasumba na watu kuathirika na mihadarati duniani amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akizungumza Alhamisi kwenye ufunguzi wa mkutano wa tatu wa ngazi ya mawaziri ujulikanao kama Paris Pact mjini Vienna , amesema nchi hiyo pia inakabiliwa na tatizo la ukimwi miongoni mwa watumiaji wa mihadarati kwa njia ya sindano.

Ban amesema dunia ina jukumu la kuwasaidia watu wa Afghanistan na wengine ambao maisha yao yako katika hali mbaya kutokana na biashara ya mihadarati. Ameongeza kuwa watu hao lazima watolewe kizani na wawe huru bila matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya na mkutano huo unapaswa kutoa muongozo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud