Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanamuziki 50 Cent aitembelea pembe ya Afrika

Mwanamuziki 50 Cent aitembelea pembe ya Afrika

Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa rap Curtis Jackson anayefahamika kama 50 Cent alikuwa na fursa ya kujionea hali alipofanya ziara nchini Somalia na Kenya. Jackson ambaye mwaka uliopita alitangaza ahadi ya kutoa chakula bilioni moja kwa watu walio na njaa amekuwa akitembelea sehemu tofauti na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ikiwemo kambi ya wakimbizi kusini mwa Somalia ambapo maelfu ya wanawake na watoto waliokimbia njaa na mapigano wamepiga kambi.

Akiwa kwenye kambi ya Kabasa Jackson alijionea wanawake wenye utapiamlo ambapo pia alizuru shule iliyokuwa karibu. Jackson pia aliitembea shule kwenye eneo la mabanda la Kiberamjini Nairobi nchini Kenya ambapo alikutana na watoto ambao wengi ni mayatima.