Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaomba dola milioni 145 kusaidia wakimbizi nchini Sudan

UNHCR yaomba dola milioni 145 kusaidia wakimbizi nchini Sudan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaitisha dola milioni 145 zaidi ili kuwasaidia wakimbizi wanaokimbia mapigano kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofa Kusini nchini Sudan na kuingia nchini Ethiopia na Sudan Kusini.

Kiasi hicho cha fedha kinalenga kuwasiadia hadi wakimbizi 185,000 kwenye nchi hizo mbili. Tangu Juni mwaka 2011 mapigano makali kati ya wanajeshi wa Sudan na kundi la Kaskazini la Sudan Peoples Liberation Movement SPLM – NORTH kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini yamesababisha zaidi ya wakimbizi 130,000 kutoka Sudan kuingia nchini Ethiopia na Sudan Kusini. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa UNHCR inawatarajia wakimbizi zaidi miezi inayokuja.