Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yaanzisha kituo kuwasaidia askari wa zamani kurejea uraiani

Sudan Kusini yaanzisha kituo kuwasaidia askari wa zamani kurejea uraiani

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vilivyoko huko Sudan Kusin vimepiga jeki uzinduzi wa ujenzi wa kituo maalumu ambacho kinakusudia kutumika kuwasaidia makundi ya askari wa zamani.

Kituo hicho kilichoko magharibi mwa nchi hiyo kitawasaidia waliokuwa askari wa zamani namna wanavyoweza kuachana na matumizi ya silaha na kuchangamana upya na jamii katika maisha ya kawaida.

Askari hao wa zamani wanatazamiwa pia kupatiwa ujunzi na mbinu za kumuda maisha wakati wanapoanza maisha mapya uraiani.

Mpango wa ujenzi wa kituo hicho unaratibiwa kwa pamoja baina ya vikosi vya Umoja wa Mataifa UNAMISS na serikali chini ya mwamvulia wa kuachia silaha.

Jumla ya askari wa zamani 500 wanatazamiwa kuanza kupatiwa mafunzo hayo.