Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya UM yamuhukumu mwanasheria wa Bosnia Serbia kwa kuidharau mahakama

Mahakama ya UM yamuhukumu mwanasheria wa Bosnia Serbia kwa kuidharau mahakama

Mahaka ya uhalifu wa vita ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya vita vya miaka ya 1990 vya Balkan leo imemuhukumu mwanasheria anayetetea Bosnia Serbia kwenda jela miezi 12 kwa kuidharau mahakama.

Mahaka inasema Jelena Rasic amepewa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia Jumanne iliyopita ya kujua na kuingilia makusudi kazi za mahakama kwa kutoa taarifa za ushahidi wa uongo kwa malipo ya fedha.

Ikitangaza hukumu yake mahakama hiyo ya Yugoslavia ya zamani ICTY imesema kwamba uhalifu ambao Jelena amekiri kuutenda ni mbaya, kwani utoaji ushahidi wa uongo katika hali yoyote ile ni kuilingia mfumo wa haki wa mahakama na katika mahakama kama ICTY una madhara makubwa.

Bi Rasic alikuwa meneja wa timu ya wanasheria wanaomtetea Milan Lukic Mserbia mwenye asili ya Bosnia ambaye alihukumiwa mwaka 2010 kwenda jela maisha kwa uhalifu uliotekelezwa Mashariki mwa Bosnia mjini Visegrad.

Mwezi uliopita Bi Rasic alikiri makosa matano ya kudharau mahakama yakiwemo kupata ushahidi wa uongo kutoka kwa Zuhdija Tabakovic kwa malipo ya Euro 1000 keshi.