Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika ziwekeze kwenye vita dhidi ya ukimwi:UNAIDS

Nchi za Afrika ziwekeze kwenye vita dhidi ya ukimwi:UNAIDS

Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS Michel Sidibe amezitaka nchi za bara la Afrika kuwekeza zaidi kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi nchini mwao. Akihutubia vingozi na serikali zilizohudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia Sidibe amesema kuwa ufadhili wa vita dhidi ya ukimwi unahitaji hatua ya nchi zenyewe ili kuyatimiza maslahi ya watu wa Afrika.

Sidibe amesema kuwa bara la Afrika limetegemea zaidi misaada suala ambalo amelitaja kuwa hatari kubwa kwa utulivu wa bara hilo. Alice Kariuki anaripoti...

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)