Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laitaka Yemen kutekeleza mageuzi ya kisiasa kwa uangalifu

Baraza la Usalama laitaka Yemen kutekeleza mageuzi ya kisiasa kwa uangalifu

 Uchaguzi ujao nchini Yemen unatazamiwa kuwa fursa na chachu ya kukaribisha kipindi cha mpito ambacho kitashuhudia uimarishwaji na kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na kukusanyisha maoni ya pande zote za siasa kwa mustabala wa taifa.

 Hayo ni kwa mujibu wa baraza la usalama ambalo limetaka kutotengwa kwa wananchi katika hatua yoyote ile wakati wa kuanzisha majadiliano ya kulijenga upya taifa hilo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, baraza hilo la usalama limekaribisha hatua ya uanzishwaji na utekelezwaji wa maazio ya kipindi cha mpito ambayo yatafanywa chini ya maridhinao yanayojulikana kama baraza la mashirikiano kwa Ghuba GCC.

 Makundi ya kisiasa yaliyotumbukia kwenye mzozo wa madaraka hivi karibuni yalitiliana saini mpango wa maridhiano na kushuhudia rais Ali Abdullah Saleh akikubali kuachia madaraka kwa makamu wake .

 Uchaguzi kwa ajili ya kupata serikali mpya umepangwa kufanyika mwezi ujao.