UM waweka historia zake kwenye mtandao

UM waweka historia zake kwenye mtandao

Mikusanyiko ya mahojiano ya Umoja wa Mataifa yaliyofanywa hadi miaka 25 iliyopita yametolewa kwa watu kwa njia ya mtandao. Uzinduzi rasmi wa mtandao huo umefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mkusanyiko wa mahojiano hayo unajumuisha karibu mahojiano 200 kuu ya warsha muhimu zilizoandaliwa tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa. Sauti za wajumbe wa zamani, wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari zinaweza kusikika kwenye mahajiano hayo.