Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kuanza kutolewa elimu juu ya tetemeko la ardhi

UM wataka kuanza kutolewa elimu juu ya tetemeko la ardhi

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakati dunia ikabiliwa na majanga ya kimaumbile yanayojiri mara kwa mara kuna umuhimu sasa kuanza kutolewa kwa elimu mahususi juu ya matetemeko ya ardhi ili kuepusha ukubwa wa madhara.

Umoja wa Mataifa umetoa zingatio hilo katika wakati ambapo ikitoa chapisho lake linaloonyesha athari mbaya zilizosababishwa na mitetemeko ya ardhi. Katika chapicho hilo inaonyesha kuwa milioni kadhaa ya watu waliathiriwa na matetemeko ya ardhi yaliyojiri katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mpya kama zilivyochapishwa na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na majanga kwa kushirikiana na kitio kimoja cha utafiti juu ya majanga, inaonyesha namna binadamu walivyoteseka kutokana na majanga hayo ya kimaumbile.

Kulingana na takwimu hizo,watu 20,943 walipoteza maisha mwaka uliopita kutokana na tetemeko la ardhi, na hii ni kati ya watu 29,782 ambao walifariki dunia kutokana na majanga mbalimbali.

Tetemeko lililoikumba Japan mwaka uliopita linasalia kuwa kielelezo cha pekee ambacho kilileta maafa makubwa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.