UM, Mataifa ya Kusin-Mashariki mwa Asia kukabili vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto

UM, Mataifa ya Kusin-Mashariki mwa Asia kukabili vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto

Wajumbe kutoka Umoja wa Mataifa na mataifa yaliyoko Kusini Mashariki mwa Asia wamekutana kwa pamoja kwa ajili ya kuainisha mikakati itayofanikisha utokomezaji wa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto. Wakikutana kwa mkutano wa siku mbili, wajumbe kutoka pande zote wamepitisha sheria na sera kwa shabaha ya kuimarisha hadhi ya makundi ya watu hao ambao wanaangukia kwenye vitendo vya unyanyasaji wa mara kwa mara.

Bi Marta Santos Pais, ambaye ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu amesema kuwa pamoja na kwamba vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto vinafanyika katika hali kificho lakini sasa hakuna njia nyingine mbali ya kusaka jawabu ya pamoja kwa shabaha ya kufichua maovu hayo.

Wajumbe hao ambao wamekutana huko Manila Philippines, wamewaalika pia wawakilishi kutoka mashirika kadhaa ya kimataifa ikiwemo UNICEF, pamoja na azimio la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na vitendo vyote vya ubaguzi dhidi ya wanawake CEDAW.