Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawataka viongozi wa Nigeria kukomesha machafuko ya kidini yanayoendelea

UM wawataka viongozi wa Nigeria kukomesha machafuko ya kidini yanayoendelea

Mashambulizi ya kupangwa na ya kidini yanayoendelea dhidi ya raia nchini Nigeria lazima yakomeshwe. Mashambulizi hayo yanayofanywa na kundi la Boko Haram na makundi mengine kwa misingi ya dini ya kabila ameonya kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay yanaweza kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Pillay amewataka viongozi wa kisiasa na kidini nchini Nigeria kuzungumza wazi kupinga machafuko hayo na kufanya juhudi muhimu za kuyakomesha. Kamisha mkuu amesema ghasia ni tishio kwa uvumilivu wa kidini ambao ni nguzo muhimu kwa umoja wa Nigeria, na kwamba kila anayechochea chuki au machafuko lazima awajibishwe bila kujali hadhi yake. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Ofisi ya haki za binadamu inakadiria kwamba zaidi ya watu 1000 wameuawa nchini Nigeria katika miaka mitatu iliyopita kufuatia machafuko ya kidini yanayotekelezwa na kundi la Boko Haram.