Hali ya watoto inaimarika nchini Haiti:UNESCO

11 Januari 2012

Hali ya watoto imeimarika nchini Haiti wakati taifa hilo likiendelea kujijenga upya baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililokumba kisiwa hicho miaka miwili iliyopita yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO linasema kufufua na kuboresha elimu ni suala linalohitaji kipaumbele. Limeongeza kuwa hivi sasa kuna watoto wengi zaidi wanaohudhuria shule kuliko ilivyokwa kabla ya tetemeko.

Kwa mujibu wa Marixie Mercado msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia watoto UNICEF, juhdi za ujenzi mpya zinachangia maendeleo na hatua zilizopigwa kwa hali ya watoto Haiti.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud