MONUSCO yalaani mauaji ya raia kijijini Kivu nchini DR Congo

10 Januari 2012

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO umelaani vikali mashambulizi dhidi ya raia yaliyofanywa na makundi ya watu wenye silaha katika vijiji vya Kivu ya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo wiki iliyopita.

Watu 45 wameuawa katika mashambulizi hayo na MONUSCO inasema imepokea taarifa kwamba watu wengine 50 wamejeruhiwa wakati kundi la wanamgambo wa Kihutu la FDLR liliposhambulia mara mbili eneo la Shabunda. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud