Shule 35 zilizojengwa kutoka kwa ufadhili wa UNICEF zafunguliwa mkoani Punjab

4 Januari 2012

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limekaribisha kufunguliwa kwa shule mpya 35 kwenye wilaya za Muzaffargah, Rajanpur na Rahimyar Khan kwenye mkoa wa Punjab wilaya zilizoathiriwa na mafuriko mwaka 2010. Zaidi ya wanafunzi 4500 kwa sasa wanahudhuria masomo kwenye shule hizo baada ya kukabidhiwa idara ya elimu kwenye mkoa wa Punjab.

Balozi kutoka ufalme wa Uholazi Hugo Sheltema alifungua shule 24 zilizofadhiliwa na Uholanzi kwenye sherehe iliyofanyika hivi majuzi. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud