Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanasayansi wa Mexico atunukiwa na shirika la UNESCO

Mwanasayansi wa Mexico atunukiwa na shirika la UNESCO

 

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO limemtunuku mwanasayansi mmoja kutoka nchini Mexico kutokana na kazi ya utafiti aliyofanya kuhusu kulala na kama mmoja wa wanasayansi waliotoa mchango kwenye masuala ya kisayansi.

Rene Raul Drucker Colin atapokea tuzo lake lijulikanalo kama “kalinga” nchini India ambalo lina lengo la kuinua sayansi. Professor huyo aliye na shahada kwenye masuala ya saikolojia anatambulika kutoka na utafiti wake kuhusu kulala na ametajwa na UNSECO kama mchangiaji mkubwa kwenye masuala ya kisayansi.