Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wa walio na matatizo ya akili hawapati matibabu kwenye nchi zinazoendelea:WHO

Wengi wa walio na matatizo ya akili hawapati matibabu kwenye nchi zinazoendelea:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa thuluthi mbili ya watu walio na matatizo ya akili kwenye nchi zinazoendelea hawapati huduma za matibabu. Kulingana na ripoti ya WHO ni kuwa uchunguzi kwenye nchi 50 zenye kipato cha chini na cha wastani uliofanywa kati ya mwaka 2005 na 2010 uligundua kuwa suala linalochangia kuwepo kwa hali hiyo ni upatikanaji wa madaktari na wauguzi wa matatizo ya akili.

Matatizo ya akili yana dalili zikiwemo za kutofikiria kwa njia inayofaa na kusikia sauti. Matatizo kama hayo huwaathiri watu milioni 26 kote duniani na kusababisha asilimia 60 ya kulemaa.