Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya UM inayoendesha uchunguzi Libya yakamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi wake

Tume ya UM inayoendesha uchunguzi Libya yakamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi wake

Tume ya Umoja wa Mataifa iliyotwikwa jukumu la kuendesha uchunguzi nchini Libya imekamilisha awamu ya kwanza ya uchunguzi huo. Tume hiyo iliutembelea mji wa Tripoli kuanzia tarehe 31 mwezi Novemba na Disemba 16 wakati inapoendelea na uchunguzi kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa vilivyotekelezwa na pande zote wakati wa mzozo nchini humo.

Mwenyekiti wa tume hiyo jaji Philippe Kirsch anasema kuwa wamefurahishwa kupata hakikisho kutoka kwa serikali inapojitolea kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu na jitihada inazofanya kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu uliofanyika nchini humo. Wakati wa ziara hiyo tume hiyo ilikutana na mwenyekiti wa baraza la kitaifa la mpito na maafisa wengine wa ngazi za juu ndani ya serikali ya Libya. Alice Kariuki ana taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)