Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urusi yataka kumalizika kwa ghasia nchini Syria

Urusi yataka kumalizika kwa ghasia nchini Syria

Urusi imewasilisha azimio kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linataka kukomeshwa kwa ghasia nchini Syria. Hili linajiri baada ya ripoti kuwa wanajeshi 27 wa Syria waliuawa na wanajeshi wa zamani waliondoka jeshini kwenye mkoa wa kusini wa Deraa.

Balozi Vitaly Chaurkin wa Urusi ambaye pia na rais wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwezi huu amesema kuwa ghasia zinazoendelea nchini Syria ni lazima zikome.

(SAUTI YA VITALY CHAURKIN)