UM watoa ombi la msaada wa dola bilioni 7.7 kwa mwaka wa 2012

14 Disemba 2011

Umoja wa Mataifa na washirika wake leo wametoa ombi la msaada wa dola bilioni 7.7 ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu milioni 51 katika nchi 16 kwa kipindi cha mwaka ujao wa 2012.

Akizindua ombi hilo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na huduma za dharura OCHA Bi Valarie Amos amesema mamilioni ya watu wataathirika na matatizo yatakayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa, upungufu wa chakula, uchumi, siasa na mengineyo na watahitaji msaada.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

Ombi hilo la msaada kwa ajili ya mwaka 2012 ni Ombi hilo limetolewa katika uzinduzi mkubwa kabisa wa ombi la msaada kuwahi kufanyika tangu kuanzishwa kwa mchakato wa kutoa maombi CAP mwaka 1991. Na linajumuisha maombi kwa ajili ya Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Djibouti, Haiti, Kenya, Niger, Somalia, Palestina, Filipino, Sudan Kusini, Yemen na Zimbabwe.

Hili sio ombi la kwanza kutolewa mwaka jana pia dola zaidi ya bilioni saba ziliombwa kwa ajili ya misaada mbalimbali na maombi hayo yamekuwa yakiwezekana kwa juhudi za mpango wa CAP kama inavyofafanua ripoti ya George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter