Wanamgambo wa Kiislam wanarudi nyuma Somalia:Ban

13 Disemba 2011

Baraza la Usalama limetolewa wito kufikiria upya utoaji wa msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya muungano wa Afrika wa kulinda amani Somalia AMISOM. Wito huu umetoka kwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon akitoa taarifa kuhusu ziara yake nchini humo wiki iliopita. Alisema kuwa wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia (TFG), wakisaidiwa na askari wa AMISOM, wamechukua udhibiti wa mji mkuu Mogadishu na kuwa wanamgambo wa Kiislam wanarudi nyuma na kwenda katika maeneo mengine ya nchi.

(SAUTI YA BAN)

Kuhusu mambo ya kijeshi, ni muhimu kuongeza askari na pia kuongeza nguvu ya AMISOM. Tunafanya tathmini ya pamoja nchini na tutarudi kwa Baraza hili na pendekezo. Wakati huo huo, narudia wito wa Umoja wa Afrika na wachangiaji wa askari za AMISOM wa kuwauliza mfikirie upya mipango ya fedha na vifaa kwa ajili ya kusaidia shughuli za AMISOM katika awamu ya pili

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter