Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICC haiwezi kusalitiwa:Ocampo

Mahakama ya ICC haiwezi kusalitiwa:Ocampo

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC haiwezi kuusalitiwa na viongozi ambao wanatishia kutenda uhalifu zaidi wakati wanatafutwa na mahakama hiyo. Amesema hayo mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno Ocampo wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwisho kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatatu.

Bwana Ocampo amesema mahakama isichukuliwe kuwa chanzo cha mijadala ya kisheria wakati inapuuzwa kunapokuja kushughulikia hali za ukiukaji mkubwa wa haki na ghasia.

Ocampo amesema ukweli unaonyesha kwamba baadhi ya viongozi wanaotafutwa na mahakama wanatishia kutenda uhalifu zaidi wakisalia madarakani, kuisaliti jumuiya ya kimataifa kwa ujanja wa madai ya uongo ya amai au haki.

Ameongeza kuwa utendaji wa mahakama utategemea jinsi gani viongozi wa kisiasa na wadhibiti wa migogoro watakavyochukulia usaliti huo.