Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Palestina waathirika pakubwa na matatizo ya uchumi ukingo wa magharibi:UNRWA

Wakimbizi wa Palestina waathirika pakubwa na matatizo ya uchumi ukingo wa magharibi:UNRWA

Ripoti mpya iliyotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA inasema licha ya habari njema kidogo katika masuala ya uchumi kwenye Ukingo wa Magharibi, idadi ya wakimbizi wasio na ajira imeongezeka karibu asilimia moja katika nusu ya kwanza ya mwaka huu na kufikia zaidi ya watu 50,000.

UNRWA inasema katika asilimia 27.4 ya watu wasio na ajira kiwango cha wakimbizi wa Kipalestina wasio na kazi ni takribani asilimia 5 zaidi ya kawaida katika Ukingo wa Magharibi. Chris Gunness msemaji wa UNRWA anasema takwimu hizi zinaonyesha kwa mara nyingine kwamba wakimbizi wa Kipalestina wanaendelea kubeba mzigo mzito wa matatizo ya uchumi katika eneo hilo.